• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Geita Town Council
Geita Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Rasilimali Watu na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Usafishaji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Nyuki na Misitu
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uchimbaji Madini
    • Sekta ya Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Elimu na Afya
      • Kamati ya Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu ya Maombi
    • Miongozo
    • Jarida la Halmashauri
    • Mkakati wa kuziwezesha
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Taasisi Za Fedha Kopesheni Kwa Riba Nafuu- DC

Posted on: March 12th, 2021

Taasisi Za Fedha Kopesheni Kwa Riba Nafuu- DC                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                    

Taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya kifedha zikiwemo benki katika Wilaya ya Geita zimeagizwa kukopesha mikopo yenye riba nafuu vikundi vya wanawake wanaojishughulisha na  ujasiriamali katika Nyanja tofauti.

Agizo hilo limetolewa na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Geita  Wakili Innocent Mabiki ambaye ni Afisa Tarafa wa Geita akizungumza kama mgeni rasmi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wanawake yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Gedeco Halmashauri ya Mji Geita.

Ndg. Mabiki amesema kuwa mikopo yenye riba kubwa ambayo inatolewa na taasisi za kifedha zilizoko katika maeneo yao zinawavunja moyo wanawake wote ambao wamekusudia kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli mbalimbali lakini wamekosa mitaji ya kuanzishishia biashara zao. Kadhalika amewakumbusha wanawake waliopata mikopo kujenga desturi ya kurejesha kwa wakati mikopo hiyo ili na wenzao wapewe.

Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Geita Ndg. Majagi Maiga ameeleza kuwa wanawake wengi katika mji wa Geita wamepata mwamko wa kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji mali ikiwemo biashara ndogo ndogo, ufugaji, kilimo cha mazao ya chakula na biashara, ushonaji nk. Dhana ya kujihusisha na uzalishaji mali imeendelea kuwafanya kuwa wabunifu wa miradi ya maendeleo.

Ndg. Maiga amesema kuwa Idara yake  hupokea baadhi ya changamoto zinazowakabili wanawake na Halmashauri ya mji wa Geita inaendelea kukabiliana nazo kwa kuendelea kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake ili kutangaza bidhaa zao na kuzikuza katika viwango vya ubora kwa kushirikiana na taasisi nyingine kama SIDO, Kuhamasisha wanawake kuunda vikundi vyenye miradi yenye mwelekeo wa viwanda vidogo na kushirikiana na wadau wa maendeleo na Taasisi za kifedha ili kuwezesha wanawake wengi zaidi kupata fursa za kuwezeshwa kiuchumi.

Siku ya wanawake duniani huadhimishwa Machi 8 kila mwaka kwa lengo la kuenzi na kutambua mchango wa wanawake katika shughuli za malezi,kijamii na kiuchumi ambazo huwezesha kusukuma gurudumu la maendeleo. Ambapo maadhimisho ya mwaka 2021 yaliongozwa na kauli mbiu isemayo “Wanawake katika Uongozi: Chachu kufikia Dunia Yenye Usawa.”




Matangazo

  • Fomu za Kuijiunga Kidato cha Kwanza Shule ya Sekndari Nyankumbu na Geita December 29, 2020
  • TANGAZO LA KODI YA MAJENGO April 20, 2018
  • TANGAZO LA WAMILIKI WA VIWANJA VILIVYOSHINDWA KUENDELEZWA BOMBAMBILI NA MAGOGO May 28, 2018
  • TAARIFA YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI YA HESABU ZA KUISHIA TAREHE 30 JUNI 2017 June 29, 2018
  • Zaidi

Habari Mpya

  • Taasisi Za Fedha Kopesheni Kwa Riba Nafuu- DC

    March 12, 2021
  • Mapato ya Ndani Kujenga Miradi ya Kimkakati

    March 04, 2021
  • Wananchi Wakumbushwa Kulipa Kodi Kwa Muda

    March 02, 2021
  • Geita Mji Yajipanga Kuepuka Mrundikano wa Wanafunzi

    February 15, 2021
  • Zaidi

Video

Bombambili Bomba ndani ya Miaka 5 ya JPM
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Applications Forms
  • Acts
  • Barua pepe za watumishi
  • Taarifa za Huduma za Afya
  • Wasiliana nasi
  • Malalamiko
  • Taarifa za Mapato

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Geita Tanzania

    Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita

    Namba ya Simu: 0282520437

    Mobile:

    Barua pepe: td@geitatc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa