Halmashauri ya Mji kupitia Idara ya Kilimo imekuwa ikisimamia na kutoa ushauri kwa wakulima juu ya uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na elimu ya ushirika kwa wanachama wa AMCOs, SACCOS na vyama vya ushirika vya msingi.
Kulingana na ardhi na hali ya hewa katika Halmashauri ya Mji wa Geita baadhi ya mazao kama Katani, dengu, tumbaku na alizeti yanaweza kustawi vizuri yakilimwa katika maeneo mbalimbali lakini wakulima hawajapata mwamko wa kuyalima isipokuwa alizeti tu ambayo inalimwa kwa kiwango kidogo sana na wakulima wachache.
Halmashauri imelenga kulima Hekta 30,340 za mazao mbalimbali ya chakula na mpaka sasa utekelezaji wake ni jumla ya Hekta 20,487 kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali.
MALENGO YA KILIMO NA MATARAJIO YA MAVUNO
Na
|
ZAO
|
LENGO( HA)
|
UTEKELEZAJI (HA)
|
MATARAJIO YA MAVUNO ( TANI)
|
1
|
Mahindi
|
7,652
|
8,458
|
19,130
|
2
|
Mpunga
|
6,078
|
3645
|
12,156
|
3
|
Mihogo
|
4,942
|
3,405
|
13,178
|
4
|
Viazi vitamu
|
3,765
|
1,531
|
12,550
|
5
|
Mtama
|
1,382
|
192
|
1,382
|
6
|
Ulezi
|
41
|
66
|
41
|
7
|
Maharage
|
3,898
|
2,022
|
3,898
|
8
|
Karanga
|
2,417
|
900
|
1,611
|
9
|
Kunde
|
360
|
268
|
360
|
MAENEO YANAYOFAA KWA KILIMO CHA UMWAGILIAJI
Halmashauri ya Mji wa Geita ina eneo la Hekta 2,870 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji kama inavyoonyeshwa katika jedwali hapo chini
Na
|
KIJIJI
|
KATA
|
UKUBWA WA ENEO( HEKTA)
|
1
|
Ibanda
|
Kanyala
|
800
|
2
|
Nyambogo
|
Shiloleli
|
650
|
3
|
Gamashi
|
Bulela
|
600
|
4
|
Nyaseke
|
Bulela
|
250
|
5
|
Bulela
|
Bulela
|
150
|
6
|
Nyakahongola
|
Kasamwa
|
170
|
7
|
Mwilima
|
Kanyala
|
250
|
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa