Idara ya Maendeleo ya Jamii ni Idara mtambuka ambayo hutekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na idara nyingine na Wadau wa Maendeleo. Shughuli zilianza kutekelezwa na idara kuanzia Novemba 2012.
Idara ya Maendeleo ya Jamii ina wajibu wa kuunganisha na kushirikisha Wananchi katika upangaji na utekelezaji wa shughuli za Maendeleo. Kujengea Jamii uelewa wa Sera, sheria na mikakati ya Maendeleo na Haki za bindamu.
Sambamba na hayo Idara hushiriki na kuratibu sherehe mbalimbali za Kitaifa na kimataifa katika maadhimisho ambayo hutoa jumbe kwa Maendeleo ya Jamii na haki za binadamu,
Idara imekuwa ikihamasisha jamii kutekeleza shughuli za uzalishaji mali katika vikundi, kuratibu utoaji wa mikopo kupitia kamati ya Mikopo iliyoundwa ili kutekeleza shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake( WDF) na Vijana (YDF) uundaji wa SACCOs ya Vijana, VICOBA na kusajiri vikundi vya kijamii CBOs lengo likiwa kuwezesha vijana na jamii kwa ujumla kujitambua na kuona thamani yao kiuchumi na kutambua fursa zilizopo ndani ya nchi yao pamoja na kuondokana na utumwa wa fikra na mtazamo juu ya suala la kuajiriwa na kuwa na uthubutu wa kujiajiri na kutengeneza ajira kwa vijana wenzao. . Uandaaji wa Mazingira na masuala ya jamii katika utekelezaji wa Miradi ya uboreshaji Mji wa Geita (ULGSP) na uboreshaji wa nyumba bora, majiko sanifu ambayo ni fursa kwa jamii kiuchumi na utunzaji wa mazingira
Idara imekuwa ikihamasisha jamii kujikinga na Maambukizi mapya ya UKIMWI na Unyanyapaa, Uhamasishaji na upatikanaji wa takwimu za Wazee, watu wenye ulemavu na watoto wanaoishi katika mazingira magumu pia hutoa huduma kwa jamii katika kushughulikia matatizo ya kifamilia ili kuleta ustawi bora wa jamii kupitia Afisa Ustawi wa Mji pamoja na kushughulikia Dawati la Malalamiko.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa