Kamati hii itashughulikia maendeleo ya ardhi, ujenzi na hifadhi ya mazingira katika eneo lake la utawala
Majukumu maalum ya Kamati
(a) Kupendekeza mipango ya kutenga maeneo ya ardhi kwa matumizi mbalimbali au mahususi,
(b) Kusimamia Mpango Mkakati wa Uendelezaji wa Mji na kudhibiti ujenzi holela,
(c) Kupitisha mapendekezo ya ramani, maeneo ya kutupa taka na taratibu nzima za usafishaji wa mji.
(d) Kupendekeza bajeti ya Mipango Miji na Mazingira pamoja na Ujenzi na Zimamoto
(e) Kupendekeza maeneo ya wazi na bustani,
(f) Kupendekeza mipango ya kutenga maeneo maalumu kwa uchimbaji wa madini,
(g) Kupendekeza mipango ya uendelezaji wa vyanzo vya maji vilima, sehemu za kujenga masoko, sehemu za kuegesha magari,
(h) Kudhibiti uchafuzi wa mazingira unaotokana na vyanzo mbalimbali
(i) Kubuni njia mbalimbali za kuendeleza utalii mjini
(j) Kuimarisha taratibu za zimamoto,
(k) Kuhakikisha ukaguzi wa majengo unafanywa mara kwa mara,
(l) Kusimamia matumizi mazuri ya barabara,
(m) Kuhakikisha kwamba majengo yote mjini yanafanyiwa ukarabati na kupakwa rangi.,
(n) Kubuni na kupendekeza majina ya mitaa na namba za nyumba katika eneo la Halmashauri,
(o) Kusimamia na kudhibiti uwekaji wa mabango,
(p) Kupendekeza Sheria Ndogo zinazohusu shughuli za Kamati
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa