Mapema leo tarehe 2 Desemba 2025, katika Ukumbi wa EPZ Bombambili, Halmashauri ya Manispaa ya Geita imefanya kikao chake cha kwanza cha Baraza la Madiwani.
Katika kikao hicho maalum, Madiwani wote wamekula kiapo cha utii, wakiahidi kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu, kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za nchi pamoja na za Halmashauri ya Manispaa ya Geita. Wameeleza dhamira yao ya dhati ya kushirikiana kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi wa Geita.
Kikao hicho pia kimeashiria mwanzo wa utekelezaji wa majukumu ya Baraza jipya, ambapo viongozi na watendaji wa Halmashauri wameonyesha mshikamano na matarajio chanya katika kipindi hiki kipya cha utawala.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa