SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA NA IDARA YA KILIMO
Kutoa mafunzo ya kanuni bora za kilimo kwa wakulima ikiwemo upandaji kwa nafasi na kwa wakati, matumizi ya pembejeo, zana na teknolojia za kisasa, teknolojia za umwagiliaji na kilimo hai. Mafunzo haya yanatolewa kwa njia mbalimbali ikiwemo mihadhara, mijadala, mashamba darasa na mashamba ya mfano.
Kutoa mafunzo ya matumizi bora ya ardhi kwenye maeneo ya kilimo kwa kupanga na kugawa matumizi ya ardhi kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kuongeza uzalishaji kwa eneo.
Kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu sekta ya kilimo, mfano ni wapi pembejeo zinapatikana, hali ya masoko, uwezesho wa kifedha na hata mashirika yanayowasaidia wakulima kupata mahitaji yao mbalimbali
Kuwasaidia wakulima kuanzisha na kutunza vitalu vya mbegu za mboga na matunda kwa ajili ya kukuza mazao ya bustani
Kufanya maonesho mbalimbali kupitia siku za wakulima, na hata ngazi ya wilaya kupitia maonesho ya nanenane.
Kutoa mafunzo ya hifadhi ya mazao ya kilimo kwa kuzingatia viwango vinavyohitajika na matumizi ya viuatilifu vya mazao ya kilimo ghalani.
Kuwatembelea wakulima, kuona changamoto wanazokutana nazo na kutoa ushauri wa jinsi ya kutatua changamoto hizo.
Kutoa tuzo na zawadi mbalimbali kwa wakulima ili kuwahamasisha wenzao kupenda kufanya vizuri zaidi. Hii inaleta ushindani ambao hatimae unasababisha ongezeko la uzalishaji kwa ujumla
Katika mwaka wa fedha 2017/2018, Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika iliidhinishiwa kiasi cha Shilingi 1,403,640,000/= kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Halmashauri ya Mji Geita. Shilingi 1,350,000,000/= kwa ajili ya ujenzi wa Skimu ya umwagiliaji Ibanda/ Igaka, Shilingi 40,000,000/= kwa ajili ya kukabiliana na Batobato kali kwenye zao la Muhogo, 13,640.000/= kwa ajili ya ununuzi wa pikipiki , ununuzi wa mbegu bora na usimamizi wa mashamba darasa.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa